Saturday, March 26, 2011

Taifa Stars kibarua kigumu leo

NI kibarua kigumu pengine kuliko vingine vyote. Hivyo ndivyo unavyoweza kuzungumziwa mchezo wa leo baina ya Taifa Stars dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati  kusaka tiketi ya kucheza  fainali za Afrika mwaka 2012.Mchezo huo muhimu wa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam unazikutanisha timu hizo ambazo zikiwa katika mazingira tofauti.

Mechi hiyo ni mtihani mwingine kwa kocha Jan Poulsen kusaka mafanikio kwa timu hiyo na kuwarejeshea imani Watanzania baada ya mchezo  wa awali  michuano huyo kufungwa na Morocco kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa nyumbani.

Kwa vyovyote vile, Poulsen ambaye ameipa mazoezi ya karibu wiki moja Stars  anahitaji matokeo mazuri leo na kuanza  kupata taswira ya ya uelekeo gani  timu yake  inao katika Kundi D, ambalo mechi nyingine itakuwa kesho kati ya Algeria na Morocco.

Afrika ya Kati ambao wanaongoza kundi hilo  watashuka dimbani chini ya kocha wao, Jules Acorsi wakitaka kuendelea kuongoza kundi kwa kujiongezea pointi zaidi ya nne walizo nazo hadi  sasa baada ya kuichapa Algeria 1-0 na kutoka suluhu dhidi ya  Morocco.

No comments:

Post a Comment