Wednesday, March 30, 2011

Hatimaye Shakira amethibisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa mwanasoka nyota Gerrard Pique baada ya kuchapishwa kwa picha zao na kumwita mwanasoka huyo kuwa ni mwanga wake mpya.
Mkali huyo wa wimbo “Hips Don`t Lie” amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa na husiano na mwanamichezo huyo tangu alipotangaza kutengana na mpenzi wake wa muda mrefu Antonio de la Rua mapema Januari mwaka huu.
Shakira aliwahi kuweka wazi kwamba alitengana na mpenzi wake kwa muda tu lakini baadaye alitangaza wazi kuwa sasa ana uhusiano na mkali huyo anayekipiga katika klabu ya soka ya Barcelona ya Hispania.
Uvumi huo ulikamilika baada ya tarehe 11 mwezi uliopita wawili hao kuonekana katika cover la gazeti la nchini Colombia la Caras wakiwa wanabusiana.
Na sasa Shakira ametangaza kuwa yupo na nyota huyo ambapo siku kadhaa zilizopita alitangaza katika ukurasa wake wa twitter huku akiweka picha ya Pique akimshika kwa mikono yake.
Sambamba na picha hiyo lakini pia Shakira ameandika kwa lugha ya kiispania “Les presento a mi sol” ikiwa na maana “wewe sasa ni jua langu".

No comments:

Post a Comment