Saturday, March 26, 2011

Jaden Smith Hajakufa!

Mwanzoni mwa wiki inayomalizika kulizuka tetesi kwamba Jaden Smith(12) amefariki, taarifa ambazo si za kweli.
Cha kusikitisha ni kwamba yeye amekuwa ni msanii wa pili kukumbwa na tetesi hizo za kifo katika siku za hivi karibuni, tetesi ambazo zimekuwa zikisambazwa kwa njia ya mtandao(internet).
Mwaka jana mshirika mkubwa wa Jaden Smith katika wimbo “Never Say Never”, Justin Bieber alizushiwa kifo kupitia mtandao wa twitter kabla ya wiki iliyopita mkali huyo wa filamu ya “Karate Kid” kukumbwa na tetesi hizo.
Pia hivi karibuni kupitia internet na Twitter kulikuwa na tetesi zilizosambaa kwamba Adam Sandler, Eddie Murphy, na Charlie Sheen wamekufa, taarifa ambazo pia zilikuwa ni tetesi tu, lakini kati ya hao watatu tetesi ya kufa kwa Sheen iliaminika zaidi.

No comments:

Post a Comment