Saturday, March 26, 2011

Samatha aipaisha Stars

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” jana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Afrika ya kati katika mchezo wa awali kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani.
Mechi hiyo ambayo Stars ilihitaji ushindi kwa hali na mali ili kujiweka sawa katika mbio hizo za kuwania fainali hizo zitakazofanyika Gabon na Equatorial Guinea ilishuhudia wenyeji wakikandikwa bao katika kipindi cha kwanza na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa nyuma,
Stars ilisawazisha dakika ya 49 kwa bao lililotiwa kimiani na Shaaban Nditi kabla ya Mbwana Samatha kufunga bao la ushindi katika dakika ya 89.
Stars ilicheza mechi ya kwanza dhidi ya Algeria ambapo ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 kabla ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Morocco ambayo ilicheza ikiwa nyumbani kwao.
Ushindi wa mechi ya jana umerejesha imani kwa watanzania kuweza kusonga mbele katika michuano hiyo muhimu kwa mataifa ya afrika.

No comments:

Post a Comment